1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISTANBUL:Jeshi lafuatilia uchaguzi kwa umakini

28 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC6N

Jeshi la Uturuki limeelezea kusikitishwa na hali ya uchaguzi wa urais katika bunge la nchini humo unavyoendelea.

Hatua hiyo inafuatia kushindwa kukamilika kwa raundi ya kwanza ya uchaguzi huo iliyoshuhudia mgombea pekee kutoka chama tawala cha Kiislam Abdullah Gul akishindwa kupata kura za kutosha.

Upande wa Upinzani usiyoongozwa na misingi ya kidini, umesusia upigaji kura na pia umeitaka mahakama ya katiba kubadilisha upigaji kura huo na kuitisha mapema uchaguzi mkuu.

Gul ambaye ni waziri wa mambo ya nje wa Uturuki, uteuzi wake umezua utata, nchini humo ambapo wengi wana wasi wasi ya kwamba huenda akaitumbukiza pabaya Uturuki.

Katika taarifa yake jeshi la nchi hiyo limesema kuwa, liko hapo kulinda mfumo wa nchi hiyo kutoegemea upande wowote wa dini na kwamba linafuatilia kwa karibu hali ya mambo.

Raundi ya pili ya upigaji kura ambayo mshindi anatakiwa kupata theluthi mbili ya kura inatarajiwa kufanyika wiki ijayo.