1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISTANBULMahakama ya katiba kuamua juu ya uchaguzi Uturuki

30 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC5m

Mahakama ya kikatiba nchini Uturuki inajiandaa kuangalia uhalali wa kufanyika uchaguzi wa rais ambao umesababisha mzozo wa kisiasa katika taifa hilo.

Mamia kwa maelfu ya watu nchini humo waliandamana hapo jana kwenye barabara za mji wa Istanbul kuunga mkono mfumo wa kisiasa usiofungamana na dini. Baadhi ya waandamanaji walibeba mabango na kupiga kelele za kukipinga chama tawala cha AK kilicho na wingi mkubwa bungeni.

Wandaamaji wanahofia kwamba endapo mgombea wa chama hicho atachaguliwa kama rais wa Uturuki basi nchi hiyo itageuka kuwa yenye kufuata misingi ya dini ya kiislamu.

Jeshi la Uturuki pia limezungumzia wasiwasi huo.

Upinzani katika bunge ulisusia uchaguzi wa duru ya mwanzo na waziri wa mambo ya nje bwana Abdulla Gul mgombea pekee wa kiti cha rais wa chama tawala alishindwa kupata uwingi wa kura kumuwezesha kushinda uchaguzi huo.