1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISTANBUL:Waziri mkuu aitisha uchaguzi wa mapema

2 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC5L

Waziri mkuu wa Uturuki Tayyip Erdogan ameitisha uchaguzi wa mapema nchini humo kuumaliza mvutano uliosababishwa na upinzani wa kutaka siasa zitenganishwe na dini.

Uchaguzi huo unaweza kufanyika juni 24.Bwana Erdogan pia amesema ataanzisha mageuzi makubwa ya taratibu za uchaguzi ikiwa ni pamoja na kuruhusu rais achaguliwe moja kwa moja na wananchi.Matamshi ya waziri mkuu yamekuja baada ya makahama ya katiba nchini Uturuki kubatilisha duru ya mwanzo ya uchaguzi wa raisi iliyofanywa bungeni wiki iliyopita.

Waziri wa mambo ya nje Abdullah Gul mwenye msimamo wa kidini kutoka chama cha AK alichaguliwa na bunge kuwa rais lakini alishindwa kupata wingi wa kumuezesha kuchaguliwa rais . vyama vinavyotaka masuala ya dini na siasa yatenganishwe viliwasilisha ombi katika mahakama ya katiba la kupinga hatua hiyo ya kuchaguliwa kwa bwana Gul kuwa rais wa nchi hiyo.

Wapinzani wa sera za dini ya kiislamu katika siasa za nchi hiyo wanahofia kwamba Gul angechaguliwa kuwa rais angeiongoza nchi kwa misingi ya kidini.