1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ivory Coast na Kombe la Afrika

16 Januari 2008

Corte d' Iviore ni makamo-bingwa wa kombe la Afrika .Wakicheza nchi jirani ya Ghana wanasema wako mnyumbani na kombe ni lao.

https://p.dw.com/p/CqtN

Ingawa nahodha wa zamani wa Black Stars-Abedi Pele,asema Ghana ndio itakayotawazwa mabingwa nyumbani katika kombe la Afrika la mataifa linaloanza jumapili hii mjini Accra,Ghana,mashabiki wa Cort d’Iviore au Ivory Coast upande wapili wa mpaka,wanaamini Mungu yuko upande wao na hivyo wameingia misikitini mjini Abidjan na katika kanisa kuu „Basilica“ mjini Yamoussukro kuwaombea dua tembo wao kuwazima Black Stars-nyota nyeusi-Ghana na kuwakanyaga simba waliobaki porini.

Dua hio zinaombwa wakati stadi wao Didier Drogba wa Chelsea,anaomba dua msimu ujao acheze bega kwa bega na mshambulizi wa Kameroun-simba wa nyika Samuel Eto’o katika la Liga-ligi ya Spian upande wa FC Barcelona.

Imam Cisse,amemgeukia Mungu badala ya waganga na wachawi wa dimba.Amenukuliwa kusema, „Tumezungumza na mola kwa moyo safi na mola daima akiitikia dua zetu.Na ndio maana ninaweka matumaini tutalinyakua kombe.“ Alisema imamm Cisse baada ya sala kwenye msikiti wa mtaa wa Treichville, mjini Abidjan,mji mkuu.

„mungu tupe ushindi,Mungu tupe kombe“ aliomba dua hizo huku mashabiki wengine mtaani wakiitikia „Amin“-ndio iwe hivyo.

Nao mama tembo-kikundi cha mashabiki akina mama walioandaa ibada hiyo ya kuwaombea dua tembo wao wanajiandaa kwa msafara wa masaa 8 barabarani hadi nchi jirani Ghana ambako wataimba,watahanikiza na kucheza ngoma za kienyeji kuiipa shime timu itakayoongozwsa na nahodha wao Didier Drogba ,stadi wa chelsea,klabu ya Uingereza ya Premier League na mchezaji bora wa mwaka 2006 wa Afrika.

Drogba kabla kuiongoza Ivory Coast huko Ghana,abainika kumnyoshea mkono wa urafiki stadi wa simba wa nyika-Kameroun Samuel Eto’o lakini sio katika kombe hili la Afrika lakini baada ya kombe hili.Alisema jana kwamba angetamni wacheze pamoja huko Spian msimu ujao katika klabu ya Barcelona .Alisema drogba, „msham,bulizi yeyote katika hali kama yake angesema angefurahi kupata nafasi kucheza bega kwa bega na Samuel Eto’0.“-drogba aliliambia gazeti la Uingereza jana Daily Express. Nae Eto’o alijibu nguvu za Drogba na kasi zangu ni mchanganyiko wa kutisha na sioni kwanini hatuchanganyiki kucheza pamoja.

Kabla kucheza pamoja huko Barcelona, mastadi hawa 2 kwanza ni maadui nchini Ghana alao hadi Februari 10 siku ya finali na ya kuamua wapi kombe linaelekea.

Tembo wa Ivory Coast walilikosa kombe dakika ya mwisho miaka 2 nyuma pale nahodha wao Drogba alipoizamisha jahazi katika mkwaju wa penalty na Misri ikalibakisha kombe mjini Cairo.

Ivory Coast baadae ilitamba katika kundi gumu kabisa kwenye kombe la dunia hapa Ujerumani 2006 ikiangukia kundi moja na Holland na Argentina.

Mjini Abidjan,bidhaa za timu ya Corte d’Iviore kama jazi na nembo ya tembo zinanunuliwa hivi sasa madukani kwa shauku kubwa.Kuanzia bendera hadi jazi za picha za stadi na nahodha wao Diduier Drogba.

Ivory Coast yenye utajiri wa kakao ingawa imegawika kati ya kaskazini-eneo linalodhibitiwa na waasi na kusini chini ya serikali kuu,katika kombe la Afrika, tembo wanapepea bendera moja tu ile ya Corte d’Iviore. Na ikiwa watarudi na kombe hadi Abidjan Februari 10, yale mapatano ya amani yaliofikiwa karibuni yatazidi kujenga umoja uliovunjika .

Ivory Coast hadi karibuni ilikua mikononi mwa kocha wa kijerumani uli Stielieke na sasa chini ya mfaransa.

Kama desturi zao pale timu yao inapocheza n’gambo, waivory Coast mara hii pia wanapanga kujenga kijiji cha mashabiki wao nchini Ghana.Huko watapika mapishi yao ,vilabu vyao vyavinywaji na muziki utahanikiza na hasa tembo wakitamba msituni si mbali na mpaka wao.

Ijinia wa mambo ya komputa Ali Konate amesema, „nitakwenda Ghana kuishangiria timu yetu na kuridi nayo na kombe kama 1992.Na wanasema, „Mramba asali,harambi mara moja.Mafiraouni wa Misri-mabingwa watawakumbusha Tembo wembe ule ule uliowanyoa cairo utawsanyoa Accra.