1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

J2 08.09.2007 News

8 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBRt

Algiers. Katibu mkuu ashutumu shambulio la bomu.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon ameshutumu shambulio la bomu la kujitoa muhanga nchini Algeria kuwa ni shambulio la kigaidi, na kusema kuwa uuaji wa raia wasio na hatia haukubaliki kwa hali yoyote ile.

Kiasi watu 19 wameuwawa katika mji wa Batna na zaidi ya 100 wamejeruhiwa katika shambulio la Alhamis kiasi cha dakika 45 kabla ya kuwasili kwa rais Abdelaziz Bouteflika katika msikiti mmoja.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limesema kuwa shambulio hilo la bomu linaonyesha haja ya kuwafikisha wale wanaohusika , waliopanga na wadhamini mbele ya sheria.

Hadi sasa hakuna aliyejitokeza kudai kufanya shambulio hilo.