1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

J2 08.09.2007

8 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBRs

Lisbon. Polisi wawataja wazazi wa mtoto aliyepotea kuwa watuhumiwa.

Polisi wamesema kuwa wazazi wa msichana mdogo raia wa Uingereza ambaye ametoweka Madeleine McCann kuwa ni watuhumiwa rasmi kuhusiana na kupotea kwa mtoto wao wa miaka minne kutoka katika hoteli waliyokuwa wamepanga nchini Ureno.

Hatua hiyo inatoa mabadiliko makubwa katika utafutaji wa mtoto huo Madeleine, ambaye alipotea kutoka nyumba waliyopanga ya mapumziko ya likizo mapema mwezi wa May.

Msemaji wa familia ya McCann amesema kuwa Kate McCann anatuhumiwa kwa kumuua mwanae kwa bahati mbaya na kuficha mwili wake kabla ya kwenda kuutupa. Hakuna mashtaka yaliyokwisha fikishwa mahakamani hata hivyo.