1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

J3 0809 News

8 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBRh

Algiers. Bomu lalipuka na kuuwa watu 17.

Kiasi watu 17 wameuwawa na wengine wengi wamejeruhiwa baada ya bomu lililokuwa katika gari kulipuka katika kambi ya jeshi inayoishi walinzi wa pwani nchini Algeria.

Shirika la habari la nchi hiyo limewanukuu maafisa wa eneo lililotokea shambulio hilo ambao wamesema kuwa mlipuko huo ulitokea katika mji wa pwani ya kaskazini wa Dellys.

Mji huo uko kilometa 50 kutoka mji mkuu Algiers.

Shambulio hilo limekuja siku mbili tu baada ya shambulio jingine la bomu kuuwa watu 20 katika kundi la watu mashariki ya Algeria ambao walikuwa wakisubiri kumuona rais Abdelaziz Bouteflika ambaye alikuwa akizuru eneo hilo.