1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JAKARTA: Ajali ya ndege Indonesia imeua watu 21

8 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCLG

Maafisa nchini Indonesia wanachunguza sababu ya ajali ya ndege ya shirika la Indonesia-Garuda, iliyotokea katika uwanja wa ndege wa Yogyakarta kisiwani Java.Watu wasiopungua 21 wamefariki na zaidi ya 100 wamenusurika wengi wao wakiwa na majeraha mabaya ya kuungua.Kwa mujibu wa maafisa,ndege hiyo wakati wa kutua ilikuwa na mwendo mkubwa.Mashahidi wamesema,ndege hiyo aina ya Boeing 737,ilishindwa kusimama kwenye njia ya ndege na iliendelea kwa kasi,hadi kwenye shamba la mpunga na ikaripuka huko.