1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JAKARTA: Indonesia yataka isaidiwe kuitafuta ndege ya abiria

4 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCdZ

Indonesia imeomba isaidiwe kutafuta mabaki ya ndege ya abiria ya shirika la Adam Air aina ya Boeing 737 iliyoanguka Jumatatu wiki hii kufuatia hali mbaya ya hewa.

Juhudi za kutafuta ndege hiyo bado zinaendelea licha ya kutatizwa na hali mbaya ya hewa, ukosefu wa vifaa, milima na maji yaliyochafuka. Ndege za jeshi la angani na meli za jeshi la wanamaji zimeendelea kuitafuta ndege hiyo lakini mpaka sasa haijaonekana.

Wakati huo huo, watu wengine 12 wameokolewa siku nne baada ya feri walimokuwa wakisafiria kuzama katika pwani ya kisiwa cha Java. Mwanamme mmoja kwa jina, Suyanto, ameokolewa pamoja na mwanawe wa kiume, Anggi, akisema walikula mkate mkavu na chakula kilichoangushwa baharini na wanajeshi.

Watu zaidi ya 200 walinusurika katika ajali hiyo ya feri.