1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JAKARTA: Mafuriko Indonesia yameua hadi watu 40

3 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCMq

Mporomoko wa ardhi uliosababishwa na mvua kali nchini Indonesia,umeua watu wasiopungua 40 na wengine darzeni kadhaa hawajulikani walipo, ikiaminiwa kuwa wamegubikwa na matope.Nyumba nzima zimesombwa na mafuriko yaliotokea katika kisiwa cha mashariki cha Flores,kufuatia mvua kubwa zilizonyesha kwa mfululizo.