1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JAKARTA: Mvua kubwa huenda zikaendelea juma zima

8 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCU7

Mafuriko katika mji mkuu wa Indonesia,Jakarta yameua watu wasiopungua 20.Vile vile takriban watu 200,000 wamepoteza makazi yao.Maafisa wanasema,mafuriko hayo ni mabaya kabisa kupata kutokea tangu miaka mitano.Katika baadhi ya maeneo mjini Jakarta,kima cha maji kimefikia mita nne.Maafisa wa utabiri wa hali ya hewa,wameonya kuwa mvua kubwa huenda zikaendelea kwa juma moja jingine katika mji mkuu Jakarta.Wasaidizi wa Chama cha Msalaba Mwekundu cha Indonesia na watu waliojitolea kusaidia,wanapeleka chakula kwa maelfu ya watu waliopoteza makazi yao.Mafuriko hayo pia yameathiri vibaya sana huduma za usafiri wa umma na sehemu nyingi za mji huo hazina umeme.