1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JAKARTA. Mvua kubwa yasababisha mafuriko

2 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCVq

Mvua kubwa imesababisha mafuriko katika mji mkuu wa Jakarta nchini Indonesia.

Barabara zimefurika na kuwalazimisha mamia ya wakaazi kubakia ndani ya majumba yao.

Tope jingi kufikia urefu wa mita 4 limezagaa na kuharibu barabara kadhaa pamoja na njia za treni zinazoelekea katika mji wa Jakarta.

Huduma ya simu imetatitizika kufuatia waya za simu za chinio kwa chini kujaa maji katika mji huo wenye takriban wakaazi milioni 9.

Wanajeshi wanawasaidia wakaazi kuondoka kutoka kwenye maeneo yaliyoathirika lakini hakuna habari zozote za watu kupoteza maisha.