1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JAKARTA: Tetemeko kubwa la ardhi nchini Indonesia

12 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBQK

Tetemeko kubwa la ardhi limetokea Sumatra nchini Indonesia.Tetemeko hilo lilikuwa na nguvu ya 7.9 kwenye Kipimo cha Richter.Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Indonesia,majengo mengi yameporomoka katika miji ya mwambao wa magharibi wa Sumatra.Vile vile majengo ya ghorofa yaliyumba katika mji mkuu Jakarta.Tetemeko hilo limetokea baharini,umbali wa kama kilomita 100 kutoka mwambao wa Sumatra.Nchi za eneo la Bahari Hindi, zimetahadharishwa na Kituo cha Marekani cha Pacifik,kinachotoa onyo la gharika la Tsunami.