JAKARTA:Hatari ya kuzuka magonjwa kufuatia mafuriko nchini Indonesia
7 Februari 2007Matangazo
Maafisa wa idara ya afya nchini Indonesia wametahadharisha juu ya hatari ya kuzuka magonjwa kutokana na maji machafu yaliyoufunika mji wa Jakarta, kufuatia mafuriko makubwa yaliyosababisha vifo vya watu wasiopungua 44. Watu wengine zaidi ya laki 3 na alfu 40 wameyakimbia makao yao katika mji huo.
Mafuriko hayo yalisababishwa na mvua kubwa zilizoanza kunyesha wiki jana.