1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JAKARTA.Watu wawili zaidi wafa kwa ugonjwa wa homa ya mafua ya ndege

16 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD2J

Watalaamu wa Afya nchini Indonesia wamesema watu wawili zaidi wamekufa na ugonjwa wa homa ya mafua ya ndege.

Hadi sasa watu 54 wameshakufa baada ya kuambukizwa virusi vya N5N1 vinavyo sababisha homa ya mafua ya ndege nchini Indonesia.

Mwanamke wenye umri wa miaka 67 kutoka eneo la Bandung katika kisiwa cha Java amekufa baada mtoto wa miaka kumi na moja kufa siku mbili zilizopita katika mji wa Jakarta.

Madaktari wamethibitisha kuwa mtoto huyo alikuwa karibu na mifugo ya ndege.