1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jamaa wa waandishi wanaozuiliwa hawataonana Iran

Thelma Mwadzaya27 Desemba 2010

Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani imeeleza kuwa hakuna uwezekano wowote wa waandishi wa habari wanaozuiliwa Iran kukutana na jamaa zao waliokwenda kuwatembelea.

https://p.dw.com/p/zq4E
Sakineh Mohammadi Ashtiani aliyehukumiwa kifo kwa kupigwa mawe.Picha: rowzane.com

Kwa mujibu wa msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani,jamaa hao hawataweza kukutana katika kipindi hiki cha Krismasi kama walivyoahidiwa na serikali ya Iran.Awali,akihojiwa na Gazeti la Bild Am Sonntag,Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani,Guido Westerwelle,alisema kuwa huenda wakakutana wakati huu.Waandishi hao wawili wa habari wa gazeti la Bild Am Sonntag walikamatwa mwezi wa Oktoba walipouwa wakiwahoji mtotto wa kiume na wakili wa Sakineh Mohammadi Ashtiani aliyehukumiwa kifo kwa kupigwa mawe.Mwanamke huyo aliye na umri wa miaka 43 alikatiwa hukumu hiyo kwasababu ya mashtaka ya zinaa.Waandishi hao wa habari waliingia Iran kw akutumia vibali vya watalii.

Mostafaie auf der Pressekonferenz
Wakili wa Sakineh Mohammadi akifanya mkutano na waandishi wa habari mwezi wa Agosti.Picha: DW