1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jamie Vardy ndiye mwanasoka bora wa mwaka

2 Mei 2016

Mshambuliaji wa klabu ya Leicester City Jamie Vardy ametangazwa mshindi wa tuzo ya mwana soka bora wa mwaka na chama cha waandishi wa kandanda Uingereza

https://p.dw.com/p/1Igam
Fußball Manchester United gegen Leicester City Barclays Premier League
Picha: Getty Images/L. Griffiths

Mshambuliaji huyo wa Uingereza alipata asilimia 36 ya kura zilizopigwa na wanahabari 290 na kuwapiku wenzake Riyad Mahrez na N'Golo Kante. Vardy mwenye umri wa miaka 29, amefunga mabao 22 ya ligi kuu ya kandanda England.

Pia alivunja rekodi ya kufunga mabao kila mechi katika mechi 11 mfululizo. Leicester City inahitaji pointi mbili pekee ili kushinda Ligi Kuu ya England lakini inaweza pia kutawazwa mabingwa iwapo Tottenham Hotspurs watashindwa kuwalaza Chelsea leo usiku.

Riyad Mahrez raia wa Morocco alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka ya PFA, ambayo mshindi hupigiwa kura na wachezaji soka ya kulipwa

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Saumu Mwasimba