1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jaribio la kigaidi: Marekani

26 Desemba 2009

Raia mmoja wa Ki-Nigeria amekamatwa kufuatia jaribio la kuilipua ndege ya Ki-Marekani.

https://p.dw.com/p/LDo8
Ndege ya shirika la ndege la Northwest imetua katika uwanja wa Detroit kutoka AmsterdamPicha: AP

Rais Barack Obama ameagiza kuchukuliwa hatua za ziada za kiusalama katika usafiri wa ndege, baada ya mtu mmoja kujaribu kulipua ndege moja ya shirika la Marekani iliyokuwa inaelekea Detroit kutoka mjini Amsterdam.  Mtu huyo ambaye anasemekana ni raia wa Nigeria, alikuwa abiria ndani ya ndege hiyo, yenye chapa AIRBUS 330 iliyokuwa imewabeba abiria 278, alizidiwa nguvu na wenzake alipojaribu kuwasha fataki wakati ndege hiyo ilikuwa inatua katika uwanja wa ndege huko Detroit. Vyombo vya habari vya Marekani, vinaripoti kuwa mtu huyo amewaambia maafisa wa usalama kuwa alitoa fataki hizo na maagizo ya kuilipua ndege hiyo kutoka nchini Yemen. Rais Obama ambaye yuko likizoni huko Haiwaii anasemekana anafuatilia matukio, lakini hajabadili ratiba yake. Taarifa kutoka shirika la ndege la Northwest zinasema raia huyo wa Nigeria amekamatwa na abiria wengine walihojiwa kufuatia tukio hilo.