1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Je, amani iko njiani Mashariki ya Kati

3 Septemba 2010

kufuatia kikao cha kwanza huko Washington

https://p.dw.com/p/P3O3
Obama apatanisha kati ya Netanyahu na AbbasPicha: picture-alliance/dpa

Duru ya kwanza ya mazungumzo mapya ya amani juu ya Mashariki ya kati imemalizika jana. Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, na Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Wapalestina , Mahmud Abbas, wamepanga kukutana tena kwa utaratibu wa kila baada ya wiki mbili. Wanakusudi kuleta ufumbuzi wa amani katika muda wa mwaka mmoja kutoka sasa.Matumaini ya maafikiano ya kihistoria kufumbua kitandawili hiki, hata hivyo, si mazuri :

Yastaajabisha: Watu 2 ambao punde tu walibidi kulazimishwa kukaa mezani kwa mazungumzo ya uso kwa uso, sasa yadhihirika mengi yalibadilika huko Washington. Sasa wanazungumzia urithi wa pamoja wa Abrahm au mtume Ibrahim. Ni kwa kushirikiana pamoja tu ndipo itawezekana umma wa pande hizo mbili kuwaongoza katika mustakbala wa kihistoria-alisisitiza waziri-mkuu Netanyahu wa Israel. Na Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Wapalestina, Mahmud Abbas, alikaribisha ajabu kabisa aliposema kuwa sasa wanataka kunyosha njia ya pamoja kuingia enzi mpya. Inalengwa kama shabaha mnamo muda wa mwaka, kufikia kile ambacho kilishindwa kufikiwa mnamo miaka 60 iliopita: Kuafikiana kati ya umma wa pande hizo mbili.

Je,ni kweli kuna nia ya kuifikia shabaha hiyo ? Na je, wanasiasa hawa wawili wana uwezo na mamlaka yanayohitajika na kuvinjari kufikia shabaha hiyo ?

Yafaa; hapo nasikitika , kuwa na shaka shaka. Netanyahu hakuwa tayari kuridhia hata kurefusha mpango wa kusiitisha ujenzi wa maskani za walowezi wa Kiyahudi katika ardhi za Wapalestina uliosimamishwa hadi Septemba 26. Anajua vyema kwamba, muungano wa sasa wa serikali yake kuchukua hatua hiyo ni mwiko.

Mahmud Abbas, nae mambo hata ni magumu zaidi: Wakati Netanyahu ikibidi aweze kufanya mageuzi katika serikali yake ili ajiandikie historia maishani mwake kwa kuleta ufumbuzi wa kitandawiki hiki, kwa Rais wa Palestina linaibuka swali: Uhalali wake wa kidemokrasi: Mamlaka yake yalimalizika muda wake miezi 6 iliopita. Na tangu mapinduzi yaliofanywa na chama cha HAMAS majira ya kiangazi 2007,Abbas hadhibiti chochote katika Ukanda wa Gaza.

Hata utayarifu wa Bw.Abbas kufikia maridhiano una shaka shaka. Hivi sasa hakuna mwanasiasa mwengine wa usoni wa Kipalestina alie tayari kuitikia madai ya Marekani kama Bw.Abbas. Lakini ndie mwanasiasa dhaifu kabisa wa Kipalestina tangu kupita muda mrefu. Jinsi alivyo dhaifu,ni vigumu hata kufikiria vipi angeweza kuyauza maridhiano yatakayofungamana na kujitolea mhanga.Kwa bahati mbaya, ni machache tu yanayotia tamaa :

Katika hayo, ni ile hali ya mipango ya kufikia ufumbuzi ilikwishapikwa tangu miaka mingi iliopita ikiwa tayari sandukuni. Hali kuwa tangu Waarabu hata Waisraeli wana hamu ya kuzima ushawishi wa Iran katika Ghuba. Na pia kuna ukweli kuwa kutokana na kuongezeka tofauti kwa vizazi viwili humo nchini, ni kuundwa tu kwa dola lao Wapalestina ndiko kutakozuwia Wayahudi kutojikuta siku moja ni wachache nchini Israel.Hizi zote zinadhihirika ni hoja nzito, lakini, hoja katika mgogoro wa Mashariki ya Kati hadi sasa hazitiwi maanani.

Mwandishi: Solich,Rainer/DW Arabisch

Mtayarishi: Ramadhan Ali

Uhariri: Miraji Othman