1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Je Ugiriki itafanikiwa kupata mkopo mwingine?

3 Oktoba 2011

Ugiriki itakosa kufikia malengo yake ya mwaka huu na ya mwaka ujao ya kupunguza nakisi kwenye bajeti yake

https://p.dw.com/p/12kjB
Wafanyakazi wa serikali Ugiriki wanapinga hatua kali za kubana matumiziPicha: dapd

Haya ni kwa mujibu wa takwimu zilizochapishwa hapo jana. Malengo hayo yaliwekwa na wakopeshaji wake, ambao ni Umoja wa Ulaya na shirika la fedha la kimataifa, IMF.

Griechenland Finanzminister Evagelos Venizelos
Waziri wa fedha Ugiriki Evagelos VenizelosPicha: dapd

Ikiwa ni sehemu ya rasimu ya bajeti ya mwaka 2012, bunge la Ugiriki pia limeidhinisha mipango ya kupunguza ajira katika sekta za serikali wakati nchi hiyo inajaribu kupata awamu nyengine ya mkopo wa euro bilioni 8 wa kimataifa.

Symbolbild Euro Rettungsschirm EU Flagge Münzen
Picha: dapd

Makato hayo huenda yakaathiri wafanyakazi 30,000 wa serikali wanaokaribia umri wa kustaafu, kwa kuwaweka wafanakazi wa akiba na baadaye kuwasimamisha kazi kwa malipo ya chini. Mawaziri kutoka nchi 17 zinazoitumia sarafu ya euro wanatarajiwa kukutana mjini Luxembourg hii leo, katika jitihada za kufikia makubaliano ya kuachiwa awamu nyengine ya mkopo ambao umezuiwa na IMF kwa mwezi uliopita.

Mwandishi:Maryam abdalla/AFP, AP, dpa, Reuters