1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jee yatatokea mapambano ya mahakamani baada ya uchaguzi?

Abdu Said Mtullya6 Novemba 2012

Katika kinyan'ganyiro cha kugombea Urais nchini Marekani,Rais Obama na mpinzani wake Mitt Romney wapo sambamba sana. Hali hiyo inakumbusha uchaguzi wa mwaka 2000 uliokuwa na utata.

https://p.dw.com/p/16dS8
Pilika pilika za wapiga kura nchini Marekani.
Pilika pilika za wapiga kura nchini Marekani.Picha: Reuters

Tofuati na utata wa wakati huo,safari hii pande zote zimejitayarisha kwa mapambano ya mahakamani.

Ikiwa mtu atauzingatia uchaguzi wa Rais uliofanyika miaka 12 iliyopita nchini Marekani kuwa kigezo, uchaguzi wa tarehe 6 (leo) unaweza kuwa kipindi cha roho juu! Kwani wakati zimebakia saa chachu tu, Rais Obama na mpinzani wake Romney wapo sambamba zaidi kuliko ilivyokuwa katika wakati kama huu katika uchaguzi wa mwaka 2000, baina ya George Bush na Al Gore.

Kwa mujibu wa kura za maoni za shirika muhimu -(Real clear Politics National Average,) Obama na Romney mpaka sasa wapo sare.

Ni wazi kwamba uchgauzi wa mwaka wa 2000 unatofautiana na uchaguzi wa mwaka huu.Obama anatetea wadhifa wake. Anawania kuchaguliwa kwa kipindi kingine. Hali ya uchumi ni mbaya zaidi. Jambo lingine la kutilia maanani ni kwamba hakuna mgombea wa watu ambae angeliweza kukaribia angalau asilimia tatu ya kura kama ilivyokuwa kwa Ralph Nader miaka12 iliyopita.

Jambo muhimu sana la kulizingatia katika uchaguzi huo vilevile ni kwamba siyo idadi ya kura zilizopigwa zitakazoamua juu ya mshindi ,bali ni wapiga kura maalamu wa mabaraza yanayoitwa electoral College.

Hata hivyo, ikiwa Obama na Romney watatoka sare,kama jinsi ambavyo sasa inavyoonekana, uchaguzi hautarudiwa kama ilivyokuwa mnamo mwaka wa 2000. Ili uchaguzi urudiwe, matokeo lazima yawe sambamba sana, yaani tofauti ya kura chache katika idadi ya alfu mbili tatu. Hayo ameeleza mtafiti wa masuala ya sheria, Profesa Rick Hasen wa chuo kikuu cha California, Irvine. Miaka 12 iliyopita George Bush alishinda baada ya zaidi ya mwezi mmoja wa mapambano ya mahakamani katika jimbo la Florida.

Alishinda kwa kuwa mbele kwa kura 537. Hata hivyo wakati huo pande zote, za Demokratic na Republican hazikuwa zimejitayarisha kwa vurumai hizo za uchaguzi. Lakini hali ni tofauti safari hii-pande zote zimejishamirisha kwa mapambano ya mahakamani.

Aliekuwa mshauri wa masuala ya kisheria wa mgombea wa chama cha demokratik, amesema chama cha Demokratik kimejifunza kutokana na yaliyotokea katika jimbo la Florida miaka 12 iliyopita.Mshauri huyo John Hardin Young amesema pande vyama vyote viwili vina mawakili katika kila jimbo wanaoufuatilia uchaguzi wote. Hata hivyo washauri wa masuala ya kisheria hawafikirii iwapo kura zitapaswa kuhesabiwa tena baada ya matokeo, kwani hali kama hiyo ni nadra katika historia ya Marekani.

Mwandishi: Knigge Michael -DW,Abdul Mtullya

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman