1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERICHO : Olmert akutana na Abbas

6 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBbY

Ehud Olmert leo amekuwa waziri mkuu wa kwanza wa Israel kutembelea mji wa Wapalestina tokea kuzuka kwa mapigano miaka saba iliopita na kukutana chini ya ulinzi mkali na Rais Mahmoud Abbas wa Wapalestina katika mji wa Jericho kuzungumzia suala la kuundwa kwa taifa la Palestina.

Akisindikizwa na helikopta mbili Olmert aliwasili akiwa kwenye msafara wa magari kwenye hoteli ya hadhi ya nyota tano ilioko mita chache tu kutoka kituo cha ukaguzi cha kudumu cha kijeshi cha Israel kwenye viunga vya mji wa Jericho.

Afisa katika ofisi ya waziri mkuu wa Israel amesema masuala mazito hayatojadiliwa hivi sasa.Olmert tayari ameondoka Jericho kufuatia mazungumzo hayo ya masaa matatu.