1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Allan Johnston atunukiwa tuzo ya heshima

5 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBlh

Mwandishi wa shirika la BBC Allan Johnstone amewasili mjini Jerusalem kufuatia kuachiliwa kwake hapo jana baada ya kutekwa nyara na kuzuiliwa katika Ukanda wa Gaza kwa muda wa miezi minne.

Johnstone anatarajia kupumzika mjini Jerusalem kwa siku chache kabla ya kwenda nyumbani Uingereza.

Kuachiwa kwa mwandishi huyo kunachukuliwa kuwa ni ushindi mkubwa kwa chma cha Hamas ambacho kinatuma ujumbe kwa jamii ya kimataifa kwamba chama hicho sio cha fujo bali pia kinauwezo mkubwa wa kutatua mizozo.

Hata hivyo maafisa wa magharibi wamesema kuachiwa kwa mwandishi Allan Johnston haimaanishi kwamba jamii ya kimataifa itakitambua au kukiunga mkono chama hicho.

Wakati huo huo Allan Johnston ametunukiwa tuzo ya heshima ya haki za binadamu na shirika la kimatiafa la Amnesty International.

Kwa mujibu wa shirika hilo mwandishi huyo ametoa mchango mkubwa katika kutoa habari zinazohusu haki za binadamu.