1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jerusalem. Condoleezza ziarani mashariki ya kati.

4 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7A1

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice yuko mjini Jerusalem kwa mazungumzo ya siku mbili na maafisa wa Israel na Palestina. Ziara yake hiyo inakuja kabla ya mkutano kuhusu mashariki ya kati unapangwa kufanywa baadaye mwezi huu.

Akiwa katika ziara yake ya nane mwaka huu ya kidiplomasia baina ya Israel na Palestina , Rice amesema anamatumaini ya kupiga hatua katika waraka wa pamoja kati ya Israel na Palestina utakaoanzisha taifa la Palestina.