1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Israel itajibu mashambulio ya Wapalestina

4 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCmb

Serikali ya Israel imesisitiza kuwa yale makubaliano yaliopatikana kati ya Israel na makundi ya Kipalestina kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza,hayatoingiza eneo la Ukingo wa Magharibi.Israel imesema,vikosi vyake katika Ukingo wa Magharibi vipo tayari kupunguza shughuli zake katika eneo hilo,lakini halitosita kuchukua hatua,dhidi ya mashambulio ya Wapalestina.