1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM : Israel kutojibu mapigo kwa hatua za kijeshi

11 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBQi

Israel haitotumia hatua za kijeshi kujibu mapigo ya mashambulizi ya roketi yanayoendelea dhidi ya nchi hiyo kutoka Ukanda wa Gaza.

Waziri wa mambo ya nje Tzipi Livni amedokeza juu ya mpango wa vikwazo dhidi ya miundo mbinu ya kiraia kama vile kupunguza usambazaji wa maji na umeme.

Ameuambia mkutano wa waandishi wa habari mjini Jerusalem ambao pia umehudhuruiwa na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Ufaransa Bernard Kouchner kwamba wana hatua za kuchukuwa ambazo sio lazima ziwe za kijeshi na kwamba ni wajibu wao kuchukuwa hatua hizo.

Livini alikuwa akizungumza masaa kadhaa baada ya roketi la kienyeji la Qassam lililofyetuliwa kutoka Ukanda wa Gaza kujeruhi takriban wanajeshi 69 wa Israel waliokuwako kwenye kambi ilioko karibu na ukanda huo.