1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Israel na Syria zikutane bila ya mpatanishi

21 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBga

Israel na Syria lazima zifanye majadiliano ya uso kwa uso bila ya kuwepo mpatanishi.Waziri Mkuu wa Israel,Ehud Olmert amenukuliwa akisema hayo kujibu pendekezo lililotolewa na Rais wa Syria, Bashar al-Assad mapema juma hili kuwa majadiliano hayo yafanywe kwa kuwepo ujumbe wa tatu.Syria ilisema,itarejea kwenye majadiliano ya amani ikiwa tu yatafanywa mbele ya mpatanishi anaeaminika na kama Israel kwanza itatoa uhakikisho kuwa itairejesha Milima ya Golan iliyoiteka katika vita vya Mashariki ya Kati mwaka 1967.