JERUSALEM: Israel yakanusha kuomba ruhusa kupitia anga ya Irak
24 Februari 2007Matangazo
Israel imekanusha ripoti ya gazeti la Uingereza kuwa imeanza kujadiliana na Marekani kuruhusiwa kutumia anga ya Irak kama uwezekano mmojawapo wa mpango wa kushambulia vituo vya kinyuklia vya Iran.Makamu waziri wa ulinzi wa Israel,Ephraim Sneh ameiambia Redio ya Israel hakuna hatua kama hiyo iliyochukuliwa.Gazeti la Uingereza la “Daily Telegraph“ likimnukulu afisa wa ulinzi wa Kiisraeli wa ngazi ya juu ambae hakutajwa kwa jina,limesema,Israel imeomba ruhusu ya wizara ya ulinzi ya Marekani-Pentagon-kutumia anga ya Iraq pindi Israel itaamua kuishambulia Iran.