1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Israel yasema azma ni kuzuia makombora

19 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC0a

Waziri wa ulinzi wa Israel,Amir Peretz amesema, Israel itaendelea na mashambulio yake ya angani dhidi ya Hamas katika Ukanda wa Gaza.Amesema,azma ya operesheni hiyo ni kuzuia makombora yanayovurumishwa na wanamgambo wa Kipalestina kusini mwa Israel.Kwa mujibu wa maafisa wa kijeshi wa Israel,mashambulio ya angani ya hivi karibuni yameteketeza ghala mbili za silaha za Hamas.Wakati huo huo Israel imesema,operesheni ya kijeshi itaendelea,ilimradi maroketi yanarushwa kusini mwa Israel.Zaidi ya Wapalestina 20 wameuawa katika muda wa juma moja lililopita. Waisraeli kadhaa wamejeruhiwa pia katika mashambulio ya makombora yaliyofanywa na wanamgambo wa Kipalestina.