1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Meya wa zamani afariki dunia

3 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCdt

Meya wa zamani wa mji wa Jerusalem, Teddy Kollek, aliyeongoza kuunganishwa kwa mji huo mnamo mwaka wa 1967 baada ya vita vya mashariki ya kati, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95.

Siku chache baada ya vita kumalizika Kollek aliamuru ukuta uliougawanya mji wa Jerusalem uvunjwe.

Wakati alipokuwa meya wa Jerusalem kwa karibu miongo mitatu, Kollek alihubiri amani baina ya waisraeli na wapalestina huku akiyazingatia malengo yao ya kitaifa.

Marehemu Teddy Kollek atazikwa kesho Alhamisi mjini Jerusalem.