1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Olmert akabiliwa na shinikizo kubwa

1 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC5a

Mwanachama wa baraza la mawaziri nchini Israel, Eitan Cabel, amejiuzulu kufuatia ripoti ya vita vya Lebanon, akisema hawezi kuendelea kubakia ndani ya serikali inayoongozwa na waziri mkuu Ehud Olmert.

Hatua hii inaongeza mbinyo dhidi ya Ehud Olmert ambaye anazidi kukabiliwa na shinikizo kubwa kutoka kwa chama chake tawala cha Kadima ajiuzulu. Hii ni kufuatia ripoti iliyotolewa na jopo maalumu nchini Israel iliyoikosoa serikali ya Ehud Olmert kwa jinsi alivyoviendesha vita nchini Lebanon.

Vyombo vya habari nchini Israel vimemnukulu mwanachama wa chama cha Kadima akisema ripoti hiyo huenda ikapendekeza waziri mkuu Ehud Olmert pamoja na waziri wake wa ulinzi, Amir Perez, wajiuzulu.

Olmert mwenyewe amesema hatajiuzulu kufuatia ripoti hiyo lakini anachukua dhamana kwa kushindwa kuyatimiza malengo ya vita vya Lebanon.