1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Olmert akutana na Abbas leo

10 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBR9

Waziri mkuu wa Israel, Ehud Olmert, anatarajiwa kukutana na rais wa mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, mjini Jeruselam hii leo.

Viongozi hao watajadili maswala ya kisiasa kuhusu maandalizi ya mkutano wa kimataifa wa kusaka amani baina ya Israel na Palestina utakaofanyika baadaye mwaka huu.

Msemaji wa Israel amesema mkutano huo wa kimataifa huenda ukafanyika mjini Jerusalem, lakini uamuzi wa mwisho kuhusiana na mkutano huo bado haujapitishwa.

Wakati haya yakiarifiwa mfalme Abdulah II wa Jordan ameonya kwamba mkutano wa kimataifa wa kutafuta amani kati ya Waisraeli na Wapalestina unaodhaminiwa na Marekani huenda usifaulu ikiwa pande zote husika katika mchakato wa amani hazitafanya maandalizi ya kutosha katika majuma machache yajayo.

Rais wa Misri, Hosni Mubarak, kwa upande wake amesema bila matayarisho mazuri na kuwa na ajenda iliyo wazi, mkutano huo utashindwa kufikia makubaliano kati ya Israel na Palestina.