1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Rais Katsav akubali makosa ya kijinsia

29 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBnQ

Rais wa Israel anaeondoka madarakani,Moshe Katsav hatoshtakiwa makosa ya ubakaji,baada ya kiongozi huyo kukubali makosa mengine aliyoshtakiwa.

Mwanasheria Mkuu Menachem Mazuz aliuambia mkutano wa waandishi wa habari mjini Jerusalem kuwa Katsav amekiri orodha ndefu ya makosa ya kijinsia,ikiwa ni pamoja na usumbufu na vitendo vya aibu.Kuambatana na masharti ya makubaliano hayo,Katsav hatotiwa ndani na atalipa faini kubwa mno.Katsav ana kinga wakati ambapo yupo madarakani,lakini amechukua livu tangu mashataka hayo kuchomoza katika mwezi wa Januari.Rais mteule Shimon Peres,atachukua nafasi ya Katsav katika kipindi cha majuma mawili yajayo.