1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM : Shughuli za ujenzi zasitishwa

12 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCSu

Shughuli tata za ujenzi karibu na mojawapo ya maeneo matakatifu kabisa mjini Jerusalem zimesitishwa.

Meya wa mji wa Jerusalem Uri Lupolianski amesema uamuzi huo umechukuliwa ili kuwapa nafasi wananchi kutathmini mipango ya ujenzi huo na kutowa maoni yao.Wiki iliopita kulizuka fujo kutokana na shughuli za uchimbaji karibu na msikiti wa Al Aqsa ambao ni watatu kwa utakatifu kwa Waislamu.

Eneo ambalo uko msikiti huo pia linatukuzwa na Wayahudi kama ni sehemu zao za kuabudia zilizotajwa na biblia.Eneo hilo katika mji wa kale wa Jerusalem ya Mashariki uliotekwa na Israel wakati wa vita vya Mashariki ya Kati vya mwaka 1967 mara kwa mara limekuwa likikabiliwa na machafuko.