1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM : Steinmeir ataka Lebanon isiingiliwe kati

4 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCmn

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir ambaye alikutana na Wariri Mkuu wa Lebanon Fouad Siniora hapo jana amesisitiza wito kwa nchi jirani za Lebanon kuheshimu haki ya nchi hiyo kujiamulia mambo yake yenyewe.

Akizungumza mjini Jerusalem na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Israel Tzipi Livni,Steinmeir amesema anapanga kumhimiza Rais Bashar al Assad wa Syria kutojiingiza katika siasa za Lebanon wakati atakapotembelea Damascus leo hii.

Waziri Mkuu wa Lebanon Fouad Siniora ambaye ameapa kutojiuzulu amekuwa akiungwa mkono na serikali za Kiarabu na mataifa ya magharibi yakiwemo Marekani,Uingereza,Ujerumani na Misri.