1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Wanajeshi 36 wajeruhiwa kwenye shambulizi la maroketi

11 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBQq

Wanajeshi 36 wa Israel wamejeruhiwa hii leo kufuatia shambulizi la maroketi. Msemaji wa jeshi la Israel amesema maroketi hayo yamevurumishwa na wanamgambo wa kipalestina kutoka Ukanda wa Gaza.

Maroketi hayo yameanguka katika kambi ya jeshi ya Zikim iliyo kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.

Hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusu majeraha waliyoyapata wanajeshi wa Israel lakini wamepelekwa kutibiwa katika hospitali na helikopta mbili na magari takriban 20 ya kubebea wagonjwa.

Shambulizi hilo limeelezwa kuwa baya zaidi kuwahi kufanywa katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita, na huenda likaongeza shinikizo dhidi ya serikali ya Israel itafute njia ya kuyamaliza mashambulizi ya maroketi yanayofanywa na wanamgambo wa kipalestina.