1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Wanamgambo wa Kipalestina wameapa kulipiza kisasi

9 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCuQ

Israel imejiweka katika hali ya tahadhari kukabiliana na mashambulio ya kulipiza kisasi huku Wapalestina wakizika raia 18 waliouwa na vikosi vya Israel katika mji wa Beit Hanoun kaskazini mwa Gaza.Wengi walikuwa wanawake na watoto.Shambulio la siku ya Jumatano limelaaniwa kote ulimwenguni.Umoja wa Ulaya umesema kuwa umefadhaishw:Marekani kwa upande wake imesema imehuzunishwa.Israel nayo ikieleza masikitiko yake imesema,kosa lilifanywa katika shambulio hilo.Jeshi la Israel limesema lilikuwa likiwalenga wanamgambo wanaoirushia Israel makombora.Wakati huo huo rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas amesma,Israel inapunguza nafasi ya kupata amani na ameutaka Umoja wa Mataifa uingilie.Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepanga kuwa na kikako cha dharura leo hii kulijadili shambulio la Israel.Kwa aupande mwingine,makundi matatu ya wanamgambo wa Kipalestina,ikiwa ni pamoja na Hamas,yamekula kiapo kulipiza kisasi.