1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Wapalestina 2 wauawa na vikosi vya Israel

22 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBgI

Wanamgambo 2 wa Kipalestina wameuliwa na wanajeshi wa Israel,kaskazini ya mpaka wa Ukanda wa Gaza.Kwa mujibu wa duru za tiba za Kipalestina watu 2 waliuawa karibu na uzio wa umeme unaozunguka Gaza,karibu na Beit Lahiya.Majeshi ya Israel yamethibitisha mapambano hayo na kusema kuwa wanajeshi walifyatua risasi,baada ya kuwagundua watu wawili wenye silaha karibu na uzio huo.Idadi ya watu waliopoteza maisha yao tangu machafuko ya Wapalestina kuanza Septemba mwaka 2000,sasa imefikia 5,790 : wengi wao wakiwa ni Wapalestina.