1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM : Waziri Mkuu Israel amtaka Rais wake ajiuzulu

25 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCYC

Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert ameungana na wito unaomtaka Rais Moshe Katzav wa nchi hiyo ajiuzulu kutokana na madai ya ubakaji na dhila za kijinsia.

Akizungumza kwenye mkutano wa usalama Olmert ambaye mwenye anachunguzwa kwa rushwa amesema kutokana na hali ilivyo Katsav hana chaguo isipokuwa kun’gatuka.

Katsav ambaye analitaka bunge limsitishe kwa muda ili aweze kukabiliana na madai hayo ipasavyo amesisitiza kwamba hatojiuzulu hadi hapo atakapofunguliwa mashtaka rasmi.Katika mkutano na waandishi wa habari Katsav aliyeonekana wazi kuwa na jazba na kukasirika amekataa madai ya ubakaji na kutumia vibaya madaraka yake na kuelezea madai hayo kuwa ni sumu na uzushi unaotisha.Pia ameshutumu polisi na vyombo vya habari kwa kushirikiana kutaka kumuangusha.

Rais huyo wa Israel amekuwa akikabiliwa na wito unaozidi kuongezeka kumtaka ajiuzulu tokea mwanasheri mkuu wa serikali nchini Israel kutangaza mipango ya kumshtaki kwa makosa kadhaa ya jinai ikiwa ni pamoja na madai ya ubakaji kutoka kwa wanawake waliokuwa wakifanya kazi naye.