1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Waziri Mkuu Olmert hatojadiliana na Hamas

26 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBoL

Waziri Mkuu wa Israel,Ehud Olmert amefutilia mbali kufanya majadiliano pamoja na Hamas,baada ya kundi hilo lenye itikadi kali za Kiislamu kutoa kaseti yenye sauti ya mwanajeshi wa Kiisraeli alietekwa nyara na wanamgambo wa Kipalestina mwaka mmoja uliopita.Katika kaseti hiyo,Gilad Shalit alie na miaka 20 amesema,hali ya afya yake inazaidi kuwa mbaya na anahitaji matibabu hospitalini.Shalit,alikamatwa na makundi kadhaa ya wanamgambo wa Kipalestina manmo mwezi Juni mwaka jana.