1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Waziri Rice kukutana na Rais Abbas

5 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C79r

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani,Condoleezza Rice hii leo atakutana na Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas.Siku ya Jumapili,Rice alikuwa na majadiliano pamoja na viongozi wa Kiisraeli katika jitahada ya kuendeleza mpango wa kuunda taifa la Palestina.

Kwa upande mwingine waziri wa nje wa Israel,Tzipi Livni amemuambia waziri mwenzake Rice kuwa Israel,kabla ya kuhakikishiwa usalama wake,haitotekeleza mpango wo wote utakaopendekezwa na Marekani.