1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM:Blair awasili Jerusalem

4 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBSd

Mjumbe maalum wa amani katika mashariki ya kati waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair amewasili Jerusalem hii leo kutathmini juhudi zinazofanywa na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmet na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas kufikia makubaliano ya mpango mpya wa amani.

Blair ambaye ni mjumbe wa pande nne zinazotafuta amani katika eneo hilo anatarajiwa kuwa huko kwa siku kumi.

Pande hizo ni pamoja na Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Marekani na Urusi.