1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM:Blair katika mkakati wake wa kwanza Mashariki ya Kati

24 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBfu

Waziri Mkuu wa Zamani wa Uingereza, Tonny Blair amenza mkakati wake wa kwanza akiwa kama mjumbe maalum wa kundi la pande nne linalosaka amani Mashariki ya Kati.

Tony Blair amewasili mjini Jerusalem kwa mazungumzo na Waziri wa Nje wa Israel Tzipi Livni.Mapema kabla ya hapo alikuwa na mazungumzo mafupi na waziri wa nje wa Jordan.

Blair pia anatarajiwa kukutana na Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert pamoja na Rais wa mamlaka ya wapalestina Mahamoud Abbas.

Hata hivyo Tony Blair hatokutana na mwakilishi yoyote kutoka chama chenye msimamo mkali cha kipalestina cha Hamas.

Akiwa ni mjumbe maalum wa kundi hilo linalojumuisha, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Marekani na Urusi ana mipaka katika majukumu yake.