1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM:Condolezza Rice ziarani Mashariki ya kati

4 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD6B

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condolezza Rice amewataka wanamgambo wa kiislamu nchini Palestina kushirikiana na rais Mahmoud Abbas akisema kwamba kundi la Hamas haliwezi kutawala katika eneo hilo.

Waziri Rice ambaye yuko mashariki ya kati amekutana na kundi la wanasiasa wa Palestina walio na msimamo wa kadri ikiwa ni pamoja na wanachama wa chama cha rais Abbas cha Fatah mjini Jerusalem.

Bibi Rice anakutana jioni hii na rais Abbas wa mamlaka ya wapalestina lakini kwa upande mwingine kabla ya mkutano huo, rais Mahmoud Abbas alifahamisha kwamba makubaliano yake ya kuunda serikali ya mseto yenye msimamo wa kadri na kundi la Hamas yamesambaratika kufuatia kuzuka mgogoro baina ya Fatah na Hamas ambapo watu 10 waliuwawa.

Kabla ya kumalizika kwa ziara hiyo atakutana na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert ambpo mazungumzo baina yao yanatazamiwa kutuwama juu ya suala la mpango wa kinukilia wa Iran.