1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM.maafisa watatu wa vyeo vya juu watuhumiwa katika kashfa ya rushwa

19 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCQk

Maafisa watatu wa vyeo vya juu nchini Israel wamelazimika kujiuzulu kutoka kwenye nyadhfa zao baada ya kuhusishwa katika kashafa ya rushwa.

Mkuu wa polisi Mosche Karadi alijiuzulu baada ya tume ya serikali ya kupambana na rushwa ilipomtuhumu kuhusika katika kundi la mafia.

Tume hiyo pia ilipendekeza afisa mwenye cheo cha juu katika jeshi la polisi Ilan Franco afutwe kazi.

Wa tatu aliyejiuzulu kufuatia tuhuma za rushwa ni mkurugenzi wa halmashauri ya ushuru nchini Israel Jacky Matza.

Wizara ya sheria nchini Israel inatafakari juu ya kuanzisha uchunguzi rasmi dhidi ya waziri wa Fedha Abrahan Hirschson.