1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM:Mazungumzo ya pande nne kufanyika Misri

21 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBpf

Mazungumzo ya pande nne ya Mashariki ya kati yanafanyika mjini Sharm el Sheikh nchini Misri wiki ijayo.Israel imethibitisha kuwa itahudhuria mkutano huo unaolenga kuimarisha uhusiano kati yake na Palestina.Hata hivyo kulingana na msemaji wa Waziri Mkuu wa Israel mkutano huo si mazungumzo ya amani.Waziri mkuu Ehud Olmert,Rais Mahmoud Abbas wa Plaestina,Rais wa Misri Hosni Mubarak na Mfalme Abdullah wa Jordan wanatarajiwa kuhudhuria kikao hicho.

Mkutano huo ni hatua kubwa kabisa ya mataifa ya kiarabu yalio na msimamo wa wastani kumuunga mkono Rais Mahmoud Abbas wa Chama cha Fatah.Chama cha Hamas kilicho na msimamo mkali wa kiislamu kimeteka Ukanda wa Gaza wiki jana.Kikao hicho kinanuia pia kuangazia tatizo linalokumba wapatanishi katika juhudi za kutafuta amani baada ya Hamas kudhibiti Ukanda wa Gaza.

Kabla ya mkutano huo Rais Mahmoud Abbas wa Fatah anatia juhudi ili kuungwa mkono huku tawi la kijeshi la chama chake la PLO liliidhinisha uamuzi wake wa kukiondoa chama cha Hamas katika serikali ya Kitaifa na kuunda Baraza la mawaziri la dharura.