1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM:Olmert apata shinikizo zaidi za kumtaka ajiuzulu

3 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC5C

Waziri wa mambo ya nje wa Israel Tzipi Livni ni afisa wa ngazi ya juu kabisa katika chama tawala cha Kadima kumtaka waziri mkuu Ehud Olmert ajiuzulu kufuatia ripoti iliyomkosoa vikali kwa jinsi alivyoendesha vita dhidi ya Hezbolla nchini Lebanon.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Jerusalem Livni amesema amemwambia bwana Olmert kwamba kujiuzulu kwakwe kutakuwa kwa manufaa ya nchi.Maafisa wengine wa juu pia wamemtaka bwana Olmert ajiuzulu. Hata hivyo waziri mkuu Olmert amesisitiza kwamba hatong’atuka madarakani. Uchunguzi wa maoni nchini humo yanaonyesha kuwa asilimia 65 ya wanaisraeli wanamtaka Olmert ajiuzulu ikiwa ni chini ya kipindi cha mwaka mmoja baada ya kuingia madarakani. Mapigano ya mwaka jana dhidi ya Hezbollah yaliyochukua muda wa siku 34 yalisababisha mauaji ya walebanon 1200 na waisrael 120.