1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM:Olmert na Abbas wakutana

16 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC9W

Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert na rais wa mamlaka ya Palestina bwana Mahmoud Abbas wamekutana mjini Jerusalem kwa mara ya kwanza baada viongozi hao kukubaliana hivi karibuni kukutana kila baada ya wiki mbili.

Makubaliano hayo yalifikiwa kufuatia ziara ya hivi karibuni katika mashariki ya kati, ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani bibi Condoleeza Rice.

Lakini habari zinasema kuwa viongozi hao wa Israel na Palestina waliepuka kuzungumzia masuala nyeti yanayohusu pande zao.