1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM:Olmert,Abbas na bibi Rice kukutana

7 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCUL

Waziri Mkuu wa Israel bwana Ehud Olmert anatarajiwa kukutana na rais wa mamlaka ya Palestina bwana Mahmoud Abbbas pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Marekani bibi Condoleeza Rice mjini Jerusalem baadae mwezi huu. Mkutano huo ni sehemu ya juhudi za kufufua mchakato wa kuleta amani katika mashariki ya kati. Pande tatu hizo zinakutana baada ya mkutano wa mjini Washington wa wawakilishi wa pande nne zinazoshuhgulikia mgogoro wa mashariki ya kati,ikiwa pamoja na Marekani,Urusi, Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya.