1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM.Polisi watumia gesi ya machozi na risasi za plastiki kuwatawanya waandamanaji

9 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCTf

Polisi wamelazimika kuingia katika maeneo ya msikiti wa Al Aqsa mjini Jerusalem ili kuwatawanya wapalestina waliokuwa wanafanya vurugu.

Polisi hao iliwabidi kutumia mabomu ya kutoa machozi na risasi za plastiki dhidi ya wapalestina waliokuwa wakirusha mawe.

Maandamano hayo yalianza kutokana na uchimbaji unaoendelea karibu na eneo la kale la Temple Mount ambalo ni eneo takatifu kwa waislamu linalojulikana kama Haram al Sharif.

Wapalestina wanapinga uchimbaji huo, wanahofia kuwa utaharibu msingi wa eneo hilo takatifu.

Utawala wa Israel umesisitiza kuwa kazi hiyo itaendelea na kutoa hakikisho kuwa hakuna uharibifu wowote utakaotokea katika eneo hilo.